• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China Southern Airlines kuzindua safari mpya Guangzhou-Nairobi

    (GMT+08:00) 2018-05-30 10:14:47

    Shirika la ndege la China Southern Airlines limesema litaanzisha safari mpya za moja kwa moja kati ya mji wa Nairobi na Guangzhou, ikiwa ni sehemu ya hatua za kampuni hiyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

    Meneja mkuu wa Shirika hilo Bw Bw. Wu Weijun ametangaza mjini Nairobi kuwa Shirika hilo ambalo kwa sasa lina safari mbili kwa wiki kati ya miji hiyo, litaanzisha safari mpya ya tatu tarehe 9 Julai.

    Bw. Wu ameongeza kuwa Nairobi imekuwa kituo kikubwa cha usafiri wa ndege barani Afrika kutokana na mtandao mkubwa wa Shirika la ndege la Kenya KQ, na shirika lake limeshirikiana na KQ ili kuhakikisha abiria kutoka Afrika nzima wanapata urahisi kusafiri kati ya China na Afrika kupitia Kenya, kwa kupanda ndege za China Southern Airlines..

    Chama tawala nchini Tanzania CCM kimemteua mdhahiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Bashiru Ally kuwa katibu wake mkuu mpya, akiziba nafasi iliyoachwa hivi karibuni na ya aliyekuwa mtangulizi wake Abdulrahman Kinana, ambaye ameamua kustaa baada ya kukitumikia chama hicho kwa miaka mingi. George Njogopa kutoka Dar es Salaam, anaarifu zaidi

    Ni takriban wiki3 tangu bwawa la Patel Solai nchini Kenya, kuvunja kingo zake na kusababisha maafa ya vifo vya watu 46, katika eneo la Nyakenyua, kaunti ya Nakuru. Ajali hiyo, imeacha makovu kwa familia nyingi zilizoathirika na sasa waliobaki wanajizatiti kujikwamua tena baada ya tukio hilo. Tom Wanjala anasimulia jinsi waathiriwa wanavyokataa kurejea kwenye mashamba yao kwa hofu ya janga kama hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako