• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ratiba kamili ya mashindano ya klabu za soka Afrika Mashariki

  (GMT+08:00) 2018-05-30 10:50:15

  Vigogo wa soka Tanzania, Simba na Yanga huenda zikakutana nchini Kenya katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup itakayochezwa Juni 7 kwenye uwanja wa Afraha mjini Nakuru.

  Ratiba ya mashindano hayo inaonyesha Yanga itakata utepe Juni 3 dhidi ya KK Home Boys endapo itashinda mchezo huo wa mtoano, itasubiri mshindi wa mechi kati ya Simba na Kariobangi Sharks utakaopigwa tarehe 4 mwezi Juni.

  Kama Simba na Yanga zote zitashinda mechi zao za kwanza zitakutana katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa Juni 7 nchini humo.

  Timu zingine za Tanzania zinazoshiriki ni JKU ya Zanzibar ambayo itacheza mechi yake ya kwanza na bingwa mtetezi Gor Mahia Juni 4, wakati Singida United itavaana na AFC Leopards.

  Bingwa wa michuano hiyo atapata tiketi ya kwenda kucheza mechi ya kirafiki ya imataifa dhidi ya Everton ya nchini Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako