• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaendelea na Maandalizi ya mashindano ya Vijana

    (GMT+08:00) 2018-05-30 10:51:22

    Shirikisho la mpira wa kikapu tanzania TBF limesema maandalizi ya michuano ya kanda ya tano Afrika kwa vijana yanaendelea Jijini Dar es Salaam. Michuano hiyo inatazamiwa kufanyika Juni 17 hadi 22 mwaka huu.

    Kwa mara ya kwanza, Tanzania itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa 12 yanayounda kanda ya tano ya Afrika. Baadhi ya Mataifa hayo ni Kenya, Uganda, Ethiopia, Burundi, Misri na Sudan.

    Rais wa Chama cha kikapu Tanzania, Fares Magesa ameiambia RFI Kiswahili kwamba katika kuelekea michuano hiyo TBF imepokea ahadi za michango kutoka kwa wadau mbalimbali.

    Aidha katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Magesa amesema TBF inatazamia kupokea vifaa vya michezo kutoka kwa wadau wa mpira wa kikapu waliopo nchini Marekani.

    Katika michuano hiyo Tanzania, itawakilishwa na timu mbili, moja ya wanawake na nyingine ya wanaume.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako