• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bado siku 15: Brazil waendelea na maandalizi

    (GMT+08:00) 2018-05-30 10:52:03

    Nahodha wa timu ya taifa ya Brazil inayojiandaa na mashindano ya kombe la dunia, Tiago Silva, amesema yeye pamoja na wenzake wako tayari kwa ajili ya mashindano hayo na wanauwezo wa kurudisha thamani na heshima ya timu ya taifa ya Brazil ambayo hadhi yake imeshuka katika kipindi kifupi kilichopita.

    Silva alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini London nchini Uingereza ambako Brazil imeweka kambi ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia, akisema wachezaji wote wako fiti kwa asilimia 100, isipokuwa Neymar ambaye bado anaendelea kujiimarisha baada ya kufanyiwa upasuaji.

    Brazil inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki na Croatia Juni 3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako