• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mechi za Kirafiki: Nigeria na DRC watoka sare ya 1-1

    (GMT+08:00) 2018-05-30 10:52:32

    Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jana imetoka sare ya magoli 1-1 na Nigeria katika mechi ya Kimataifa ya kirafiki iliochezwa mjini Port Harcourt.

    Nigeria (Super-Eagles) ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao, kupitia beki wake William Troost-Ekong akipokea pasi kutoka kwa mshambualiaji Ogenyi Onazi, hata hivyo DRC walisawazisha kwa njia ya penati kupitia Issam Mpeko.

    Nigeria ilitumia mechi hiyo kama maandalizi ya michuano ya kombe la dunia, itakayoanza tarehe 14 mwezi Juni nchini Urusi.

    Nigeria imepangwa katika kundi C lenye timu za Argentina, Croatia na Iceland.

    Kikosi hicho kinaondoka siku ya Jumanne kwenda Uingereza, kwa maandalizi zaidi na inatarjiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki tarehe 2 mwezi Juni.

    Katika matokeo mengine ya mechi za kirafiki:

    Ureno 2-2 Tunisia

    Ufaransa 2-0 Ireland

    Korea 2-0 Honduras

    Uturuki 2-1 Iran

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako