• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya kimataifa ya biashara ya huduma ya Beijing yapongezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje

  (GMT+08:00) 2018-05-30 17:56:50

  Waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan hivi karibuni kwenye mkutano wa kilele wa maonesho ya 5 ya kimataifa ya biashara ya huduma ya Beijing, alisisitiza kuharakisha kufungua zaidi soko la huduma kwa nchi za nje. Wafanyabiashara wanaohudhuria maonesho hayo wameipongeza China kwa kufungua mlango zaidi katika sekta ya huduma, na kutaka kuongeza ushirikiano zaidi na China.

  Kampuni ya UNO Parks ya Lithuania inayoshughulikia mitambo ya bustani za michezo iliingia nchini China mwaka 2013, na hadi sasa imefanya miradi sita ya bustani ya michezo nchini China. Mwakilishi wa kampuni hiyo Bi Zhao Na, amesema pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" limeiletea kampuni hiyo soko jipya. Amesema,

  "Kutokana na pendekezo la 'Ukanda Mmoja na Njia Moja', nchi za Ulaya ya mashariki zinashiriki kwenye shughuli zinazoandaliwa na China mara kwa mara kama vile maonesho ya kimataifa ya biashara ya huduma ya Beijing. Ingawa Lithuania ni nchi ndogo yenye watu milioni 2.8 tu, lakini ina bustani 20 za michezo. China inatarajiwa kuwa na bustani za aina hiyo zaidi ya laki moja, na litakuwa soko kubwa sana kwetu."

  Ofisa wa ubalozi wa Ireland nchini China Bw. Lin Zhi amesema, madhumuni ya ubalozi huo kutuma ujumbe kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa ya biashara ya huduma ya Beijing ni kujulisha watu wa China kuhusu uhodari wa sekta ya huduma ya Ireland zikiwemo huduma za fedha, elimu na utalii, na kuhimiza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Amesema,

  "Kwa mfano wa huduma ya fedha, Ireland ni kituo kikubwa cha tano cha huduma za fedha barani Ulaya. Serikali za China na Ireland zimeanzisha mfuko wa uwekezaji katika shughuli za sayansi na teknolojia, na mwaka huu zinatarajiwa kuanzisha mfuko mwingine wenye ukubwa wa Euro milioni 150. Tunatumai kuwa kupitia mifuko hiyo miwili, kampuni nyingi za kisayansi za China zitawekeza nchini Ireland, huku kampuni za Ireland zikiweza kuingia nchini China."

  Hivi sasa China inaharakisha kufungua mlango katika sekta za elimu, afya, matunzo ya wazee, fedha, bima na uhasibu. Naibu mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa utafiti wa maendeleo na mageuzi ya China Bw. Liu Shijing ameeleza kuwa bado kuna pengo kati ya China na nchi zilizoendelea katika sekta za huduma, kufungua mlango kutaileta China fursa ya kujifunza. Amesema,

  "Badala ya fedha, tunahitaji zaidi vitu vingine kama vile teknolojia, uzoefu wa uendeshaji, na utaratibu. Vitu hivyo ni muhimu kwetu katika mchakato wa kuboresha sekta zetu ya huduma."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako