• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwenyekiti wa ICRC atajaria kuimarisha ushirikiano na China katika kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja

  (GMT+08:00) 2018-05-30 18:12:59

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu Bw. Peter Maurer ambaye yuko ziarani nchini China, ameeleza matumaini ya kuimarisha ushirikiano na China katika ujenzi wa pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja.

  Bw. Maurer ambaye yuko ziarani hapa China, amesema hayo jana alipozungumza kuhusu mgawanyiko wa maarifa na ushirikiano kati ya mashirika ya binadamu ya kimataifa na makampuni ya China, na amefafanua maoni yake kuhusu pendekezo la China la Ukanda Mmoja na Njia Moja.

  Amesema hivi sasa ICRC inafanya shughuli za kibinadamu kwenye nchi zaidi 80 duniani zikiwemo nchi zaidi ya 40 zilizoko kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja zikiwemo katika mabara ya Asia, Afrika na Ulaya. Bw. Maurer amesema kamati hiyo inapenda kubadilishana uzoefu wake na China hasa katika kupanga sera husika na maendeleo ya ofisi za serikali na makampuni na kusaidia kuhimiza ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako