• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kufanya uchaguzi wa rais Julai 30

    (GMT+08:00) 2018-05-30 18:20:56

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ametangaza Julai 30 kuwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini humo.

    Rais Mnangagwa ametangaza hivyo kupitia waraka maalum wa serikali uliochapishwa hii leo. Waraka huo umetangaza kuwa tarehe hiyo pia utafanyika uchaguzi wa wabunge na wa serikali za mitaa.

    Rais Mnangagwa pia amesema duru ya pili ya uchaguzi wa rais itafanyika Septemba 8 mwaka huu, kama atakosekana mgombea atakayeshinda kwa asilimia 50 ya kura.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako