• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza Marekani kutimiza ahadi yake na kufuata taarifa ya pamoja kati yake na China

    (GMT+08:00) 2018-05-30 18:21:00

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema, taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Marekani imekwenda kinyume na makubaliano yaliyofikiwa kati ya China na Marekani mjini Washington.

    Amesema kama Marekani itaendelea kushikilia kitendo hicho, China itachukua hatua kidhabiti kulinda maslahi yake halali. China siku zote inatetea kutatua mkwaruzano wa kibiashara kwa njia ya mazungumzo, ambayo inaendana na maslahi ya kimsingi na ya muda mrefu ya nchi hizo mbili na wananchi wao, pia ni matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.

    Habari zinasema, ikulu ya Marekani imetoa taarifa kuwa, Marekani itatangaza orodha ya bidhaa muhimu za teknolojia ya viwanda za China yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50, na kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako