• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-05-30 19:15:41

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Bibi. Hua Chunying amesema, China inapenda kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati katika pande zote kati yake na Afrika Kusini kwenye msingi wa mwanzo mpya wa miaka 20 tangu kuanzisha uhusiano wa kibalozi kwa nchi hizo mbili.

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi atafanya ziara nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwezi ujao na kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa nchi za kundi la BRICS. Bibi Hua amesema katika ziara hiyo, Bw. Wang Yi atajadiliana na Afrika Kusini kuhusu rais Xi Jinping wa China kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za kundi la BRICS, na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika hapa Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako