• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema uchumi wa China unaendelea vizuri, mageuzi katika sekta muhimu yapata maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-05-30 19:20:22

    Mkurugenzi msaidizi wa idara ya Asia na Pasifiki ya IMF Bw. James Daniel leo hapa Beijing amesema, uchumi wa China umeendelea vizuri, na mageuzi katika baadhi ya sekta muhimu yamepata maendeleo.

    Bw. Daniel amesema, maendeleo ya mageuzi katika baadhi ya sekta ni pamoja na kuharakishwa kwa kazi ya kukinga hatari dhidi ya sekta ya mambo ya fedha, kupungua kwa kasi ya ongezeko la utoaji mkopo, kupungua kwa uzalishaji unaopita kiasi, nguvu za kudhibiti uchafuzi zimeongezeka, na mchakato wa kufungua mlango unaendelea.

    Amesema kutokana na mafanikio ya mageuzi ya China katika miaka 30 iliyopita, na ahadi na nia dhabiti ya serikali ya China, anaamini China itatimiza kubadili uchumi wake kuwa wa uwiano, na kugeuza kuelekea njia ya maendeleo endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako