• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Wafanyakazi 3,000 katika sekta isiyo rasmi kunufaika na mradi mpya

    (GMT+08:00) 2018-05-30 19:49:04

    Takriban wanawake na vijana 3,000 pamoja na biashara ndogo ndogo 600 zinatarajiwa kunufaika na mradi wa miaka mitatu ambao unatekelezwa na Shirika la Kimataifa la Leba (ILO) na washirika mbalimbali.

    Mradi huo uliopewa jina "Kukuza kazi nzuri katika sekta isiyo rasmi Rwanda" unalenga kuwawezesha wanawake na vijaana zaidi ya 3,000 ,pamoja na kuimarisha uwezo wa biashara ndogo ndogo 600 zinazofanya kazi katika sekta isiyo rasmi.

    Mradi huu ulizinduliwa jumatatu wakati wa mkutano ambao uliwaleta pamoja maafisa wa ILO,Wizara ya Leba na Utumishi wa Umma,na wadau kutoka taasisi mbalimbali nchini Rwanda.

    Mratibu wa Kitaifa wa ILO,Jude Muzale alisema lengo kuu ni kuchangia katika utoaji wa fursa za ajira nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako