• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanasoka Mrisho Ngassa asajiliwa tena na klabu ya Yanga ya Dar es salaam

    (GMT+08:00) 2018-05-31 08:31:36

    Habari kutoka Dar es salaam zinasema klabu ya Yanga ya Dar es salaam imeimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili mchezaji wake wa zamani Mrisho Ngassa, hii ni siku chache baada ya kuenea kwa tetesi kuwa klabu hiyo imeyumba sana kiuchumi kiasi cha kushindwa kufanya usajili wa nafasi tatu za wachezaji watakaoongeza nguvu katika kikosi cha Kombe la shirikisho Afrika. Mrisho Khalfan Ngassa aliwahi kuichezea Yanga kwa miaka kadhaa kabla ya kuamua kwenda Free State ya Afrika Kusini, Fanja FC ya Oman, Mbeya City ya Mbeya na baadae akajiunga na Ndanda FC kabla ya kutangazwa kurudi tena Yanga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako