• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wachezaji wa Uingereza wateta kuhusu hatua watakazochukua wakifanyiwa ubaguzi wa rangi Russia

    (GMT+08:00) 2018-05-31 08:33:19
    Wachezaji wa Uingereza wamezungumzia kuhusu hatua watakazochukua iwapo wenzao watabaguliwa kwa vigezo vya rangi katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia, inayotyarajiwa kuanza baada ya wiki mbili. Hatua hiyo inafuatia kuendelea kwa vitendo vya ubaguzi wa rangi, l;icha ya kampeni za mara kwa mara dhidi ya vitendo hiyo. Hivi karibuni shirikisho la soka la Russia lilipigwa faini ya £22,000 kwa kelele za ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa, mchezo uliochezwa mwezi machi. Mchezaji mwandamizi wa timu ya taifa ya Uingereza Ashley Young, amesema wakati unapokuwa uwanjani kuna wakati hujui la kufanya, lakini wamezungumza kuhusu swala hilo na uamuzi utakaochukuliwa kama hilo litatokea kwa wachezaji wa timu yao.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako