• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mario Balotelli arudi kwenye timu ya taifa ya Italia

  (GMT+08:00) 2018-05-31 08:54:08

  Mwanasoka mwenye matata wa Italia Mario Balotelli amerudi kwa kishindo kwenye timu ya taifa ya soka ya Italia, na kuisaidia timu yake kufunga goli moja kati ya magoli mawili ilipocheza na timu ya Saudi Arabia kwenye mechi ya kirafiki, Hii ni mara ya kwanza kwa Balotelli kuicheza Azzurri tangu mwaka 2014. Lakini kama ilivyokawaida Mario hukumbwa na mikasa ya ajabu, na safariri hii alikumbwa na vitendo vya ubaguzi, baada ya shabiki mmoja kuonekana na bongo lenye maneno "nahodha wa timu yangu ana damu ya Italia". Lakini Mario alijibu kupitia ukursa wake wa Instagram akisema amkeni huu ni mwaka 2018. Balotelli mzaliwa wa Italia ambaye wazazi wake ni waghana, amechaguliwa na kocha wa Azzurri Roberto Mancini kuwa nahodha msaidizi wa Azzurri!"

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako