• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa mataifa alaani kupamba moto kwa mapambano huko Gaza

    (GMT+08:00) 2018-05-31 09:10:11

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia mchakato wa amani wa Mashariki ya kati Bw. Nickolay Mladenov amelaani mapambano yanayotokea kwenye ukanda wa Gaza. Bw. Mladenov ameliambia Baraza la usalama kuwa siku mbili zilizopita Ukanda wa Gaza umeshuhudia mapambano makali zaidi tangu mgogoro kati ya kundi la Hamas na Israel uanze mwaka 2014, na kuonya kuwa mapambano hayo yakiendelea yatabadilika kuwa vita. Kauli hiyo imekuja baada ya makundi ya Hamas na Jihad kurusha maroketi 216 dhidi ya Israel Jumatatu na Jumanne, na jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya anga dhidi ya shabaha 65 za makundi hayo kwenye ukanda wa Gaza kulipiza kisasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako