Serikali ya Marekani inapanga kutoza ushuru wa adhabu kwa bidhaa za chuma cha pua na alumini zilizoingizwa kutoka Umoja wa Ulaya. Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal, Marekani inatarajiwa kutangaza hatua hiyo leo hii, ambayo gazeti hilo limesema ni hakika kuwa Umoja wa Ulaya utaijibu kwa hatua za kukipiza kisasi ikiwemo kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za Marekani kama vile pikipiki, nguo za jeans na pombe ya Bourbon. Wiki iliyopita serikali ya Marekani pia ilianzisha uchunguzi wa usalama wa taifa dhidi ya vipuri vya magari, ambao unaweza kufanya kuongezwa kwa ushuru dhidi ya magari yanayoingizwa kutoka Ulaya.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |