• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kushughulikia migogoro ya ardhi kati ya vijiji na kambi za jeshi

    (GMT+08:00) 2018-05-31 10:17:03

    Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa wa Tanzania Bw. Hussein Mwinyi amesema serikali imekuwa ikichukua hatua zinazolenga kutatua migogoro ya ardhi kati ya vijiji na kambi za jeshi.

    Akihutubia bunge mjini Dodoma Bw. Mwinyi amesema serikali ina wasiwasi na kuongezeka kwa wimbi la migogoro hiyo, na imepanga kufanya utafiti wa kitaifa kuhusu suala hilo ili kuchukua hatua madhubuti. Ameongeza kuwa migogoro hiyo imeripotiwa kutokea katika sehemu nyingi nchini Tanzania na inahitaji kushughulikiwa.

    Bw. Mwinyi amesema hayo alipojibu swali lililoulizwa na mbunge wa Morogoro Mjini Abdul Azizi Abood, ambaye alitaka kujua ni lini serikali itatatua migogoro ya ardhi kati ya wakazi wa vijiji vya Kauzeni na Kuhongo katika mkoa wa Morogoro, na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako