• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini afanya ziara Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-05-31 10:17:27

    Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amefanya ziara nchini Ethiopia na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Abiy Ahmed.

    Rais Kiir aliyeambatana na mpatanishi mkuu wa amani wa Sudan Kusini na mawaziri wa serikali, anatarajiwa kutoa ripoti kwa waziri mkuu wa Ethiopia kuhusu nafasi ya Sudan Kusini katika mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Nchi za Afrika Mashariki IGAD. Ethiopia ni mwenyeji wa mazungumzo hayo yanayolenga kurudisha makubaliano ya amani ya Sudan Kusini yaliyosainiwa mwaka 2015 na baadaye kusimamishwa.

    Wakati huohuo, msemaji wa serikali ya nchi hiyo Bw. Michael Makuei amesema Marekani kuweka vikwazo dhidi ya maofisa wa serikali ya rais Kiir hakutaondoa nia ya serikali ya kutimiza amani nchini humo. Kauli imekuja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutarajiwa kupiga kura leo kuhusu kuwawekea vikwazo maofisa waandamizi wa serikali ya Sudan Kusini akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako