• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupunguza zaidi ushuru kwa bidhaa za matumizi ya kila siku

    (GMT+08:00) 2018-05-31 10:26:49

    China itapunguza zaidi ushuru wa bidhaa za matumizi ya kila siku zinazoingizwa kutoka nje kuanzia mwezi Julai mwaka huu.

    Mkutano wa baraza la serikali uliofanyika jana chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu wa China Bw Li Keqiang, umeamua kupunguza kwa zaidi ya nusu ushuru wa kuagiza bidhaa za nguo, viatu, kofia, vyombo vya jikoni, vifaa vya michezo na mazoezi, na vifaa vya matumizi ya nyumbani kama majokofu na mashine za kufulia nguo.

    Baraza hilo limesema hatua hiyo inaweka mazingira mazuri ya kupanua ufunguaji mlango, kukidhi mahitaji ya wananchi na kuboresha viwanda. Taarifa ya baraza inasema China itatoa hatua nyingine zaidi za kuweka mazingira ya haki zaidi, wazi zaidi na rahisi zaidi kwa uwekezaji wa makampuni kutoka nje, na kulinda zaidi maslahi ya wawekezaji kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako