• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hadithi 9 kuhusu urafiki kati ya rais Xi Jinping na watoto wa China na wa nchi mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-05-31 15:36:46

    Tarehe 1 Juni ni sikukuu ya watoto ya kimataifa. Rais Xi Jinping siku zote anafuatilia ukuaji wa watoto na vijana.

    1. Baba anayempenda mtoto wake

    Rais Xi Jinping si kama tu ni rais wa China, bali pia ni baba anayempenda mtoto wake.

    Kwenye rafu ya vitabu ya ofisi yake, kuna picha inayoonesha kwamba anapanda baiskeli pamoja na mtoto wake.

    2. Babu anayeona haya

    Mwaka 2014 aliongea na watoto zaidi ya 10 katika mtaa wa Junmen mjini Fuzhou. Msichana Zou Ruining mwenye umri wa miaka 7 aliandika kuwa "Babu Xi anaona haya sana!" Ukweli ni kwamba haoni haya, anapenda sana watoto.

    3. Rais Xi aliwaandikia barua watoto

    Kabla ya sikukuu ya watoto mwaka 2016, wanafunzi 12 wa shule ya msingi mjini Taizhou alimwandikia barua rais Xi Jinping. Rais Xi alijibu, "Natarajia mtakuwa wajenzi wapya wa taifa wenye ujuzi, maadili na mafanikio."

    4. Aliwahi kulia kwa sababu kushindwa kujiunga na Shirikisho la Chipukizi mapema

    Rais Xi alisema aliposoma katika shule ya msingi ya Minzu ya eneo la Haidian mjini Beijing, alishindwa kujiunga na Shirikisho la Chipukizi katika kikundi cha kwanza, na alilia. Wakati aliposhiriki kwenye shirikisho hili, alikuwa na furaha kubwa moyoni.

     

    5. Rais Xi anakumbuka watoto wanaoishi katika eneo lililokumbwa na maafa

    Tetemeko kubwa la ardhi lilitokea tarehe 20 Aprili mwaka 2013. Rais Xi aliwatembelea watoto wanaoishi huko. Mtoto Luo Juncheng mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alimwita babu na kumbusu. Babu Xi pia alimbusu.

    6. Urafiki kati ya Rais Xi Jinping na watoto wa Australia

    Mwaka 2014, wanafunzi 16 wa shule ya msingi kutoka Tasmania, Australia aliwaandikia barua rais Xi Jinping na mkewe Peng Liyuan, na kuwalika kutembelea makazi yao. Rais Xi na mkewe walitembelea huko, na wanafunzi hao walihudhuria hafla ya kuwakaribisha.

    7. Rais Xi ni mshabiki ya soka

    Mwaka 2014 rais Xi alipofanya ziara nchini Ujerumani, alikwenda uwanja wa michezo mjini Berlin, na kuwatembelea wachezaji vijana wa soka waliopata mafunzo kule. Rais Xi alisema "Nina matarajio makubwa kuhusu nyinyi, natumai mtakuwa wachezaji maarufu duniani!"

    8. Wanafunzi wa shule ya msingi wa Pakistan awakaribisha rais Xi kwa kutoa matangazo kwenye gazeti

    Mwaka 2015, wanafunzi wa shule ya msingi ya Roots Millennium walitoa matangazo yenye picha na maneno ya kichina kwenye gazeti kuwakaribisha rais Xi kufanya ziara nchini humo.

    9. Kuwa wanasayansi ni ndoto ya watoto wengi wa China

    Rais Xi Jinping alipohudhuria mkutano wa wajumbe wa taasisi ya sayansi ya China na taasisi ya uhandisi ya China, rais Xi Jinping aliwaambia wanasayansi wa China kwamba kuwa wanasayansi ni ndoto ya watoto wengi wa China, tunahitaji kuifanya sayansi iwe kazi inayowavutia watoto, na kutimiza ndoto yao, ili China iwe na wanasayansi wengi katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako