• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wateja wa China waongeza kununua bidhaa zilizotengenezwa kwenye nchi za nje

    (GMT+08:00) 2018-05-31 16:41:31

    Wizara ya biashara ya China hivi karibuni imetoa takwimu kuhusu bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za nje, zikionesha kuwa wateja wa China wanapenda kununua bidhaa zilizotengenezwa nchi za nje, na zaidi ya asilimia 30 ya wateja wanapanga kuongeza kununua bidhaa hizo katika miezi sita ijayo, wakati huo huo kampuni za China pia zinataka kuongeza maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje.

    Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, mahitaji ya wateja wa China kwa bidhaa zilizotengenezwa nchi za nje yanaongezeka, kati ya watu waliohojiwa, zaidi ya asilimia 20 wananunua bidhaa kutoka nchi za nje kwa kutumia asilimia zaidi ya 30 ya matumizi yao ya bidhaa zote. Sababu kuu ya hali hii ni ubora wa bidhaa zilizotengenezwa katika nchi za nje. Wateja wamesema,

    "Mtoto wangu anapenda vitu vya kucheza na vyakula kutoka nchi za nje."

    "Sina wasiwasi kuhusu usalama na ubora wa vyakula na bidhaa nyingine kutoka nchi za nje."

    Takwimu hizo zinaonesha kuwa, katika miezi sita ijayo, zaidi ya asilimia 30 ya wateja wa China wanapanga kuongeza kununua bidhaa zilizotengenezwa nchi za nje, na bidhaa zinazowafurahisha zaidi ni vipodozi, saa za mkononi, miwani, vitu vinavyohitajiwa na mama na mtoto mchanga, magari na vito. Naibu mkurugenzi wa idara ya utafiti wa soko la kimataifa ya wizara ya biashara ya China Bw. Bai Ming anaona kuwa, kutokana na ongezeko la uwezo wa kiuchumi, wateja wa China wanazingatia zaidi ubora wa bidhaa. Amesema,

    "Zamani vipato vya wachina ni vidogo, wanatilia maanani zaidi bei. Hivi sasa wanazingatia zaidi ubora wa bidhaa."

    Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa kampuni za China zitaongeza maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje, haswa pombe, matunda mabichi, nguo za michezo, vyakula vya watoto wachanga, vipodozi, saa za mkononi na magari.

    Katika miaka ya hivi karibuni, China imefungua milango zaidi kwa bidhaa za nchi za nje, na kupunguza ushuru wa forodha hatua kwa hatua. Takwimu zilizotolewa na wizara ya biashara ya China zinaonesha kuwa, hadi mwezi Januari mwaka huu, China imesamehe ushuru wote wa forodha kwa bidhaa za aina zaidi ya 8000.

    Mkurugenzi wa idara ya utafiti wa ushirikiano wa kikanda ya wizara ya biashara ya China Bw. Zhang Jianping ameeleza kuwa, kuongeza maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje si kama tu kunaweza kukidhi mahitaji ya wateja, bali pia kutahimiza maendeleo ya uchumi. Amesema,

    "Kwa kuwa China imegeuka kuwa nchi yenye mapato ya kiwango cha katikati, mahitaji ya watu kwa bidhaa yanaongezeka siku hadi siku. Tunaongeza maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje, ili kukidhi mahitaji hayo. Aidha, ongezeko la maagizo ya bidhaa kutoka nchi za nje pia litahimiza maendeleo ya uchumi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako