• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China yasema orodha hasi kurahisisha zaidi ukomo wa uwekezaji wa kigeni

    (GMT+08:00) 2018-05-31 18:08:12

    Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China Gao Feng amesema, China inafanyia kazi orodha mpya hasi kwa upatikanaji wa uwekezaji wa kigeni katika soko.

    Gao amesema hayo leo hapa Beijing alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Amesema vizuizi katika maeneo ya nishati, miundombinu, uchukuzi, mzunguko wa biashara na huduma za kitaaluma vitaondolewa au kurahisishwa katika orodha ijayo. Tayari China imetangaza hatua za kulegeza masharti katika sekta za fedha na utengenezaji wa magari.

    Wakati huohuo, Tume ya Biashara ya Manispaa ya Beijing imesema, mji huo ni makao makuu ya kampuni zaidi ya elfu 4. Mkurugenzi wa Tume hiyo Yan Ligang amesema makao makuu hayo yana asilimia 50 zaidi ya mali kuliko ilivyokuwa mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako