• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Kenya yalenga kustawi katika biashara ya mafuta kabla ya kuwaza faida

    (GMT+08:00) 2018-05-31 18:55:22

    Serikali ya Kenya inalenga kujistawisha kwenye biashara ya kimataifa ya mafuta kwanza kabla ya kuwaza faida kubwa ya fedha zitakazopatikana.

    Kwa mujibu wa katibu mkuu wa wizara ya kawi nchini Andrew Kamau ,licha ya Kenya kuanza rasmi kusafirisha mafuta katika bandari ya Mombasa jumapili wiki hii,wanazingatia zaidi utaratibu mzima wa usambazaji wa mafuta hayo pamoja na viwango kwenye soko la kimataifa.

    Kenya itauza mafuta hayo kwa bei ya chini ikilinganishwa na nchi nyingine kwani itauza viwango vichache vya mafuta kwa majaribio.

    Kila siku mapipa elfu 2 ya mafuta yatasafirishwa hadi Mombasa kutoka Lokichor Turkana.

    Hata hivyo kufikia mwaka 2021 ,Kenya ituza zaidi ya mapipa elfu 80 ya mafuta kwa siku.

    Asilimia 5 ya mapato ya biashara ya mafuta yatatumika kuwafaidi jamii ya Turkana,asilimia 20 zitaenda kwa kaunti ya Turkana nayo serikali kuu itachukua mapato ya jumla ya asilimia 75.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako