• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lafanya mkutano wa dharura kuhusu suala la Palestina

    (GMT+08:00) 2018-05-31 18:59:35

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limefanya mkutano wa dharura kuhusu suala la Palestina, ambapo mratibu maalumu wa umoja huo kwenye mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov ameripoti hali ya sasa kati ya Palestina na Israel.

    Kwenye mkutano huo, balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu amesema, China inafuatilia sana hali ya Palestina, hasa wasiwasi wake kuhusu hatari ya mgogoro kwenye sehemu ya Gaza kuzidi kuwa mbaya. Amesema China inazitaka Israel na Palestina zijizuie na kusitisha operesheni za kijeshi, ili kusuluhisha hali ya kanda hiyo.

    Wakati huo huo, Bw. Ma amesisitiza kuwa China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, na kutoa mchango kwa ajili ya amani ya Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako