• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa uchumi wa Afrika asema uchumi wa Afrika unahitaji matumizi zaidi ya sarafu ya China

    (GMT+08:00) 2018-06-01 09:38:54

    Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Uchumi na fedha ya nchi za mashariki na kusini mwa Afrika MEFMI Bw. Caleb Fundanga, amesema kuna haja ya kutumia sarafu ya China kama sarafu ya akiba kwa kuwa China inatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa nchi za Afrika.

    Akiongea kwenye mkutano wa baraza la wataalamu wa fedha uliofanyika wiki hii kuwakutanisha manaibu magavana wa benki kuu na manaibu mawaziri wa fedha wa nchi 14 zilizo chini ya taasisi hiyo, Bw Fundanga amesema wataalam hao wamekubaliana kuwa wakati umefika kwa sarafu ya China kuwa sarafu ya akiba.

    Maoni kama hayo yamefikiwa kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa China kwenye maswala ya biashara barani Afrika. Bw. Fundanga amesema nchi za Afrika zinaweza kutumia sarafu ya China kama fedha ya akiba kama inavyofanya kwa Euro na Dola ya Marekani, Na kufanya hivyo kunaweza kusaidia nchi za Afrika zisiathiriwe na mabadiliko ya viwango vya thamani ya sarafu hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako