• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyefichua mpango wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu Russia asema amemtambua mwanasoka mmoja wa Russia

    (GMT+08:00) 2018-06-01 09:44:26

    Zikiwa zimebaki siku 13 kabla ya fainali za kombe la dunia kutimua vumbi nchini Russia, aliyekuwa ofisa wa Russia aliyefichua kashfa ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu amezusha tafrani baada ya kusema anamtambua mmoja wa wachezaji wa Russia. Grigory Rodchenkov ambaye amepewa hifadhi nchini Marekani, ndiye alifichua mpango kabambe wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa timu ya Russia iliyoshiriki kwenye michezo ya majira ya baridi ya Sochi. Amesema kati ya majina ya kikosi cha Russia anafahamu jina moja kwenye mpango huo, lakini hakusema kama ni mchezaji au ni ofisa. Wachezaji wote wa Russia wameidhinishwa na FIFA kuwa wako safi. Hata hivyo wataendelea kupimwa kama wachezaji wengine wote katika kipindi cha kombe la dunia, na sampuli zitapelekwa Uswisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako