• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa real Madrid Zenedine Zidane amejiuzulu nafasi yake

    (GMT+08:00) 2018-06-01 09:44:52

    Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi ikiwa ni siku tano tangu aipe timu yake taji la ubingwa mara ya tatu mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Zidane anaagana na Real Madrid kwa heshima baada ya kuitumikia kwa miaka miwili. Mfaransa huyo alithibithisha leo mchana kwamba ataachia nafasi hiyo kama kocha mkuu wa Real Madrid licha ya kuipataia mafanikio makubwa klabu hiyo. Mkongwe huyo wa soka mwenye miaka 45, baada ya kutwaa ubingwa wa Uefa ilikuwa inatabiriwa angeongezewa mkataba hadi mwaka 2020. Hata hivyo awali kulikuwa na presha kubwa kutoka uongozi wa Madrid kutokana na kutofanya vyema kwenye La Liga msimu huu ulioisha. Makocha Arsene Wenger, Pochetino wa Tottenham, na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Low, pamoja na Antonio Conte aliyeluwa Chelsea, ni miongoni mwa wanaotajwa kumrithi Zidane, huku Conte akipewa nafasi kubwa Zaidi. Zidane alirithi mikoba ya kocha Rafael Banitez Januari 2016 na msimu huo huo aliipa taji la Ligi ya Mabingwa timu hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako