• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga na Simba zaelekea Kenya kwenye Kombe la Sports Pesa Super cup

    (GMT+08:00) 2018-06-01 09:45:41

    Watani wa jadi Yanga na Simba za Tanzania, wameelekea Nairobi Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup yanayokishirikisha timu 8, na kufanyikia huko Nakuru. Chachu ya ushindi wa mashindano hayo, inatokana na zawadi nono inayotolewa na SportPesa kwa Bingwa wa michuano hiyo kupelekwa mjini Liverpool England kucheza dhidi ya Everton katika uwanja wa Godson Park. Michuano ya SportPesa Super Cup itaanza June 3 hadi June 10 2018. Yanga wapo Kundi moja na timu za Home Boys, Gor Mahia na JKU ambao ni Mabingwa wa Zanzibar. Simba wameondoka wakiwa na wachezaji wao wa kikosi cha kwanza kama Aishi Manula, Shomari Kapombena Erasto Nyoni kitu ambacho kinaonesha kuwa wamedhamiria kutwaa Ubingwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako