• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanariadha wa Tanzania Francis Damas amesema atajitahidi kupata medali kwenye mbio za kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-06-01 09:46:00

    Mwanariadha, Francis Damas wa Tanzania amesema ana matumaini ya kutwaa medali ya dhahabu kwenye mbio za dunia za vijana zilizopangwa kufanyika nchini Finland. Damas atachuana Juni 16 katika mbio zitakazofanyika Jamhuri ya Czech kusaka viwango vya kushiriki mashindano ya dunia yaliyopangwa kuanza Julai 10 hadi 15. Francis ambaye ni mshindi wa medali ya shaba katika michezo ya Madola mwaka jana nchini Bahamas, anatarajiwa kuondoka Tanzania Juni 10 kwenda Jamhuri ya Czech. Mwanariadha huyo anatarajiwa kuchuana katika mbio za mita 3000 na 5000 kwenye mashindano hayo na akifanya vyema ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya dunia ya vijana. Kocha wa mwanariadha huyo, Meta Petro alisema maandalizi ya Damas yako katika hatua nzuri na ana matumaini ya kufanya vyema katika mashindano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako