• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa dola bilioni moja kwa ajili ya mradi wa kupanua kituo cha umeme Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:03:38

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema China imeipatia Zimbabwe fedha kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa kituo cha umeme cha Hwange, ambacho ni kikubwa zaidi nchini humo.

    Fedha hizo zimetolewa baada ya rais Mnangagwa kukamilisha ziara yake nchini China mwezi Aprili. Imefahamika kuwa mradi huo utakaotekelezwa na kampuni ya China Sinohydro unatarajiwa kuongeza megawati 600 za umeme kwenye gridi ya taifa ya Zimbabwe.

    Konsela wa biashara wa China nchini Zimbabwe Bw. Li Yaohui amethibitisha kutolewa kwa fedha hizo, na kusema China imeipatia Zimbabwe dola milioni 200 za kimarekani, na nyingine dola milioni 800 pia zitatolewa ndani ya muda mfupi. Amesema hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo inatarajiwa kufanyika katikati ya mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako