• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa mwandamizi wa DPRK kukabidhi barua ya Rais Kim Jong Un kwa Rais Trump

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:03:57
    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw Mike Pompeo amesema ofisa mwandamizi wa Korea Kaskazini anapanga kwenda Marekani na kuwasilisha barua ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kwa rais Donald Trump.

    Bw. Pompeo amesema hayo katika mkutano na wanahabari mjini New York baada ya kumaliza mazungumzo ya siku mbili na ujumbe wa Korea Kaskazini unaoongozwa na naibu mwenyekiti wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyakazi cha Korea Kaskazini Bw. Kim Yong Chol.

    Bw. Pompeo amesema maendeleo yamepatikana kwenye mazungumzo na Korea Kaskazini yaliyofanyika mjini New York na sehemu nyingine. Lakini amesema bado hajui kama mkutano wa marais wa nchi hizo mbili utafanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni kama ilivyopangwa.

    Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeripoti kuwa kiongozi Kim Jong Un amesema dhamira yake ya kuondoa silaha za nyuklia haibadiliki. Aidha, wizara ya mambo ya muungano ya Korea Kusini imesema maofisa wa ngazi ya juu wa Korea Kusini na Korea Kaskazini leo watafanya mazungumzo katika kijijji cha Panmunjom.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako