• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaadhimisha mwaka mmoja wa reli ya SGR

    (GMT+08:00) 2018-06-01 10:35:15

    Wananchi wa Kenya wameadhimisha mwaka mmoja wa reli ya SGR, huku ikiendelea vizuri na huduma zake kusifiwa na watumiaji wa reli ambao ni wasafiri wa kawaida, wajasiriamali na watalii.

    Akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho hayo kwa niaba ya waziri wa uchukuzi na miundombinu wa Kenya Bw. James Macharia, meneja mkurugenzi wa Kampuni ya Reli ya Kenya Bw. Atanas Maina amesema katika mwaka mmoja uliopita, reli ya SGR imeziletea mapinduzi usafiri wa watu, bidhaa na huduma nchini humo. Pia amesema tangu mwanzo, reli hiyo iitwayo Madaraka Express imejitahidi kupunguza gharama za usafiri na kuwafanya Wakenya wapate huduma wanazoweza kumudu, ziwe rahisi na za uhakika.

    Kampuni ya ujenzi wa Barabara na madaraja ya China imetekeleza mradi wa ujenzi wa SGR ambao ni matokeo ya mwanzo ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja. Pendekezo hilo lilitolewa na China mwaka 2013 kwa lengo la kujenga mitandao wa biashara na miundombinu inayounganisha Asia na Ulaya na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako