• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atumia barua ya pongezi kwa Mkutano wa kwanza wa vyombo vya habari wa SCO

    (GMT+08:00) 2018-06-01 11:40:54

    Mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari wa Shirika la ushirikiano wa Shanghai SCO umefanyika leo mjini Beijing, ambapo rais Xi Jinping wa China ametumia barua ya pongezi.

    Kwenye barua hiyo rais Xi amesema, hivi sasa kiwango cha mawasiliano ya habari kimepata maendeleo kwa kasi, na vyombo vya habari vimeonesha umuhimu mkubwa katika kuhimiza mawasiliano ya watu wa nchi mbalimbali siku hadi siku. Lengo la pendekezo alilolitoa mwaka mmoja uliopita kuhusu kuandaa mkutano huo wa kwanza wa vyombo vya habari ni kuhimiza mawasiliano kati ya nchi wanachama wa SCO katika sekta ya utamaduni.

    Rais Xi amesema China inaunga mkono kwa hatua madhubuti maendeleo ya SCO, pia inapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye kanda hiyo na ya binadamu wote.

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ambaye pia ni mkuu wa idara ya uenezi ya chama hicho Bw. Huang Kunming ametangaza barua ya rais Xi Jingping kwenye ufunguzi wa mkutano huo. Kauli mbiu ya mkutano huo ni Kueneza moyo wa Shanghai na kufungua zama mpya ya ushirikiano kati ya vyombo vya habari. Wajumbe zaidi ya 260 kutoka idara za mawasiliano na vyombo vikuu vya habari vya nchi wanachama wa jumuiya hiyo wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako