• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga mfumo wa kuwasaidia watoto walemavu kupona

    (GMT+08:00) 2018-06-01 17:06:52

    Kuanzia tarehe mosi, Oktoba mwaka huu, China itajenga mfumo wa kuwasaidia watoto walemavu kupona, na kutoa msaada wa gharama za upasuaji, vifaa na huduma za mazoezi kwa watoto walemavu wenye umri wa chini ya miaka 6 kutoka familia maskini.

    Kupona kwa watoto walemavu kunamaanisha baada ya kutokea kwa ulemavu, watoto hao wanasaidiwa kupunguza athari za ulemavu, na kuongeza uwezo wa kuendesha maisha na kushiriki kwenye shughuli za kijamii, kwa njia za matibabu, elimu, saikolojia na vifaa vya kusaidia. Takwimu zinaonesha kuwa hivi sasa nchini China kuna watoto walemavu wenye chini ya umri ya miaka 6 karibu milioni 1.68. Naibu mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Walemavu la China Bw. Xia Yong amesema, utoto ni kipindi kizuri cha kupunguza athari za ulemavu, kupitia hatua madhubuti za kugundua, kutibu na kusaidia mapema, watoto wengi wanaweza kuongeza uwezo wa kukabiliana na ulemavu. Hali ambayo itapunguza mzigo wa kiuchumi na kisaikolojia ya familia zao, na kuwasaidia watoto hao kusoma na kufanya kazi kama watu wa kawaida. Bw. Jia amesema,

    "Watoto walemavu watakaosaidiwa ni pamoja na wale wasio na uwezo wa kusikia, kuona, kuongea, akili na viungo. Mbinu kuu ni kuwasaidia kupunguza athari, kuongeza uwezo wa kujihudumia maishani na kushiriki kwenye jamii."

    Bw. Jia amesema kwa mujibu wa mfumo wa kuwasaidia watoto walemavu kupona, serikali pia itawasaidia watoto walemavu kutoka familia maskini na mashirika ya hisani kupata matibabu ya upasuaji, vifaa na huduma za kufanya mazoezi ya kupona. Amesema,

    "Hivi sasa hatua halisi za mfumo huo haswa ni kuwapatia watoto wasioweza kusikia vifaa ya kusikilizia na kuwasaidia kufanya mazoezi husika, kuwasaidia watoto wenye kasoro ya viungo kufanya upasuaji na kuwapatia vifaa ya kusaidia, na kuwasaidia watoto wenye matatizo ya akili kufanya mazoezi ya kutambua na kujihudumia maishani."

    Habari zinasema bajeti ya mfumo huo itatengwa na serikali za mitaa, na serikali kuu pia itatoa ruzuku. Hadi kufikia mwaka 2020, watoto wote walemavu watakaokidhi vigezo watasaidiwa kutokana na mfumo huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako