• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yautaka mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa kuheshimu nchi wenyeji

    (GMT+08:00) 2018-06-01 18:35:08

    China imeutaka mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa kuheshimu matakwa ya nchi wenyeji katika kutoa misaada ya maendeleo.

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Ma Zhaoxu ametoa wito huo baada ya Baraza Kuu la Umoja huo kupitisha azimio kuhusu kurekebisha mfumo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa. Azimio hilo linatoa jukumu kubwa kwa wawakilishi wa kikanda kuongoza na kusimamia nchi wenyeji, na kuweka wazi kuwa nchi zilizo kwenye mpango zina kauli ya mwisho kuhusu Mfumo wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa.

    Balozi Ma amesema, kipengele cha uteuzi wa wawakilishi wa kikanda kinapaswa kuamuliwa kutokana na mawazo ya nchi wanachama kwa kuendana na kipaumbele na mahitaji ya nchi inayopatiwa msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako