• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yatoa wito kutatua tofauti za kibiashara kwa njia ya ushirikiano wa kiujenzi

    (GMT+08:00) 2018-06-01 18:47:57

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetoa wito kutatua tofauti za kibiashara kwa njia ya ushirikiano wa kiujenzi.

    Msemaji wa shirika hilo Gerry Rice amesema, ingawa ongezeko la biashara linaendelea kusaidia katika kufufua uchumi wa dunia, lakini mvutano wa kibiashara pia unaendelea kuwa mbaya zaidi.

    Bw. Rice amesema, IMF inahimiza nchi mbalimbali kupunguza vizuizi vya kibiashara na kutatua tofauti za kibiashara kwa ushirikiano halisi na kutochukua hatua kali. Amesema, vita ya kibiashara ya muda mrefu itaharibu maslahi ya pande zote.

    Habari zinasema, serikali ya Marekani imeamua kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma na alumini kutoka Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako