• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yawarejesha wavuvi 46 wa DRC waliokamatwa kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na makundi ya wapiganaji

    (GMT+08:00) 2018-06-01 19:03:21

    Uganda imewarejesha wavuvi 46 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao walikamatwa kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na makundi ya wapiganaji yaliyowateka nyara raia sita wa Uganda mwezi uliopita.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema, wavuvi hao wamekabidhiwa kwa mamlaka ya DRC katika mji wa mpaka wa pamoja wa Kasese jana jioni. Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya uamuzi wa mahakama moja mjini humo kuwaachia huru wavuvi hao na kuwarudishia boti yao ya uvuvi na injini, baada ya kila mmoja wao kulipa faini ya dola za kimarekani 83.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako