• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa sekta ya nyumba watakiwa kutrumia teknolojia zilizoidhinishwa

    (GMT+08:00) 2018-06-01 19:15:54

    Serikali ya Kenya imewaonya wawekezaji wa nyumba dhidi ya kutumia teknolojia za ujenzi ambazo hazijaidhinishwa wakati wanapoweka juhudi za kujenga nyumba za gharama nafuu. Akitoa onyo hilo, mkuregenzi mkuu mtendaji wa KEBS Bw Charles Ongwae amesema ingawa wamekuwa wakihimiza sekta ya nyumba kukumbatia teknolojia za kisasa za ujenzi kuna haja ya wadau kwenye sekta ya nyumba kuhakikisha teknolojia wanazotumia ni salama na pia zimeidhinishwa na Mamlaka hiyo. Hatua hii inakuja wakati ambapo nyumba nyingi zimekuwa zikiporomoka na kusababisha vifo na majeruhi kwa wakenya wengi. Miongoni mwa Teknolojia ambazo zimeidhinishwa ni pamoja na matumizi ya paneli na matofali ya kuchombwa ambayo mara nyingi hutumiwa katika maeneo ya vijijini. Kwa muda wakenya wamekuwa wakitumia mfumo wa ujenzi sawa na wa Uingereza lakini katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakikumbatia wa Ulaya. Serikali tayari imehimiza taasisi za mafunzo ya kiufundi kuanza kutumia mfumo huo wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako