• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wa Uganda kuanza kulipia kodi ya Mitandao ya kijamii

    (GMT+08:00) 2018-06-01 19:16:14

    Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp.

    Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata Jumatano.

    Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda kila siku. Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa 1% ya thamani yake.Tayari wabunge watatu wa Uganda wamekosoa sheria hizi mpya na kuzitaja kama "utozaji wa kodi mara dufu. Kuna mkanganyiko mkubwa kuhusu namna ushuru huo mpya kwa mitandao ya kijamii utakavyotekelezwa. Wataalam pamoja na watoaji wa huduma za Intaneti wameelezea hofu yao juu ya sheria hiyo mpya. Mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu ya kisiasa nchini Uganda kwa chama tawala na upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako