• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yakusanya mrabaha mara tatu zaidi kutokana na ukuta karibu na mgodi

    (GMT+08:00) 2018-06-01 19:17:37

    Waziri wa Madini nchini Tanzania, Angellah Kairuki, amesema ujenzi wa ukuta unaozunguka mgodi wa madini ya Tanzanite, umewezesha Serikali kukusanya mrabaha mara tatu zaidi ya ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita. Wizara hiyo ambayo sasa imetenganishwa na Nishati, imeliomba Bunge kuidhinisha Shilingi bilioni 58.9 kwa ajili ya matumizi yake ya mwaka 2018/19, hilo likiwa ni ongezeko la Sh6.5 bilioni ikilinganishwa na bajeti iliyopita.

    Waziri Kairuki ameongeza kuwa kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 19.6 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 39.2 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

    Amesema ukuta ambao ujenzi wake ulianza Novemba 1, 2017 na kukamilika Februari 15 umeongeza mapato, na kubainisha kuwa katika kipindi kifupi cha Januari hadi Machi, 2018 wizara ilikusanya jumla ya Shilingi bilioni 714.6. Alisema kati ya fedha hizo, Tsh614.7 milioni zinatokana na makusanyo kutoka kwa wachimbaji wadogo .Mwaka wa 2015, Serikali ya Tanzania likusanya mrabaha wa shilingi bilioni 166.9 milioni, 2016 shilingi bilioni 71.9 milioni na mwaka 2017 ilipata Sh147.1 milioni kutoka kwa wachimbaji wadogo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako