• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 47 wameuawa na wengine 54 wakijeruhiwa kwa mwezi uliopita pekee nchini Libya

    (GMT+08:00) 2018-06-02 18:16:09

    Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Libya UNSMIL, jana limetoa ripoti inayoeleza kuwa, kwa mwezi Mei pekee mwaka huu raia 47 wameuawa na wengine 54 wakijeruhiwa kutokana na vurugu.

    UNSMIL imewataja waathirika hao wapatao 101 kuwa walitokana na vitendo vya vurugu za kiuhasama, ikiwemo mabomu yalitegwa kwenye magari na yale ya kujitoa mhanga katika maeneo mbalimbali ya nchini Libya.

    UNSMIL walikamilisha ripoti hiyo kwa kuzitaka pande zote za Libya ziache matumizi ya silaha za moto na silaha zingine zisizo za moja kwa moja na matumizi yasiyosahihi ya mabomu ya kurushwa hewani kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu, na wasipeleke wapiganaji au vikundi vya kijeshi katika maeneo yenye watu wengi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako