• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Duru ya 8 ya Mazungumzo ya kimkakati ya ngazi ya juu kati ya China na Ulaya yafanyika

    (GMT+08:00) 2018-06-02 18:19:43

    Mjumbe wa taifa wa China ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko Brussels ameendesha duru ya 8 ya mazungumzo ya kimkakati ya ngazi ya juu kati ya China na Ulaya pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya diplomasia na sera za usamala Bw. Federica Mogherin.

    Bw. Wang Yi amesema kuwa, China inapenda kushirikiana na Umoja wa Ulaya kufanya maandalizi ya mkutano wa 20 wa viongozi wa China na Umoja wa Ulaya, ili kuhakikisha mkutano huo unapata mafanikio, na kuonyesha ishara ya China na Umoja wa Ulaya kujitahidi kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, kulinda na kuimarisha utaratibu wa kimataifa. China inapenda kuongeza zaidi hali ya kuaminiana kisiasa kati yake na Umoja wa Ulaya, kuzidisha ushirikiano wa uchumi na biashara, kuhimiza uwekezaji na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja", na kuimarisha ushirikiano wa pande nyingi.

    Bw. Federica Mogherin amesema, upande wa ulaya unakubali maoni ya China, na kupenda kushirikiana na China kuzidisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote, kuimarisha uratibu wa kimkakati, kukabiliana kwa pamoja na changamoto , kulinda na kuimarisha mfumo wa ushirikiano wa pande nyingi unaoongoza Umoja wa Mataifa na utaratibu wa kimataifa wenye msingi wa kanuni. Hayo yanaendana na maslahi ya pande mbili na maslahi ya dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako