• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya waadhimisha miaka 55 ya uhuru kukiwa na tumaini pamoja na changamoto

    (GMT+08:00) 2018-06-02 18:26:09

    Wakati huu ambapo wakenya wanasherehekea miaka 55 ya kujitawala wenyewe, jambo moja ambalo linawasumbua wananchi ni kwamba nchi bado pambana na changamoto ilizokuwa nazo wakati wa uhuru.

    Changamoto hizo ni pamoja na mgawanyiko wa kikabila, umaskini, ukosefu wa ajira na ufisadi ulioenea kwenye maeneno yote ya jamii.

    Viongozi na wananchi kwa pamoja wanatambua ukweli kwamba Kenya imechukua hatua za kupunguza au kumaliza matatizo hayo ambayo yanarudisha nyuma.

    Maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya uhuru yanafanyika kukiwa na ongezeko kubwa la kashfa za rushwa kwenye idara nyingi za kiserikali ambazo zimesababisha chuki ya umma na ubeuzi dhidi ya utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.

    Katika maadhimisho ya siku ya uhuru ijumaa hii, wananchi walisubiri kwa dhati kusikia Rais atatoa msimamo gani kuhusu mapambano dhidi ya ufisadi, kujenga umoja baina ya watu, uanzishwaji wa ajira na kuhusu umaskini.

    Katika hotuba yake, Kenyatta aliwahakikishia wananchi kwamba serikali yake itafanyakazi kuhakikisha nchi inafikia malengo.

    Tangu achaguliwe kwa mara ya pili amekuwa akifanya juhudi ili kuleta umoja baina ya watu na juhudi katika mapambano dhidi ya rushwa, ambapo katika wiki iliyopita serikali yake iliwafanyia uchunguzi watu wapatao 40 waliohusishwa na tuhuma za rushwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako