• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai na kuunga mkono Korea Kaskazini na Marekani ziendane kwa mwelekeo wa pamoja

    (GMT+08:00) 2018-06-02 19:31:55

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying leo hapa Beijing amesema kuwa, China inatumai na kuunga mkono Korea Kaskazini na Marekani kuendana na mwelekeo wa pamoja, na kusukuma mbele maandalizi ya mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

    Bibi Hua Chunying amesema kuwa, mara nyingi China imesisitiza kuwa, hali ya peninsula ya Korea inakabiliana na fursa nzuri ya kihistoria, mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili ni muhimu kwa kupata njia ya kutimiza peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia na amani ya kudumu. China inatumai kuwa, pande mbili za Korea Kaskazini na Marekani zitasukuma mbele maandalizi ya mkutano wa viongozi, na kujitahidi kutimiza matokeo yanayotarajiwa na pande mbili na jumuiya ya kimataifa, ili kutoa mchango kwa ajili ya kutimiza lengo la kuifanya peninsula ya Korea kuwa sehemu isiyo na silaha za nyuklia, amani na ustawi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako