• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa taarifa kuhusu mashauriano kati yake na Marekani juu ya masuala ya uchumi na biashara

    (GMT+08:00) 2018-06-03 14:26:47
    China imetoa taarifa kuhusu mashauriano kati yake na Marekani juu ya masuala ya uchumi na biashara yaliyofanyika Jumamosi na Jumapili hapa Beijing, na kwamba mashauriano hayo yalipata maendeleo mazuri kuhusu masuala kadhaa yakiwemo kilimo na nishati, na matokeo juu ya mambo halisi yanasubiri kukubaliwa na pande hizo mbili.

    Naibu waziri mkuu wa China Liu He na waziri wa biashara wa Marekani Wilbur Ross wakiongoza timu zao za kikazi, walijadiliana kwa msingi wa makubaliano yaliyofikiwa kati yao mwezi Mei huko Washington, Marekani.

    Taarifa hiyo imesema, ili kukidhi mahitaji ya watu wa China na kufanikisha maendeleo ya uchumi wake, China inapenda kuongeza manunuzi ya bidhaa kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, hatua ambayo inanufaisha watu wa nchi hizi mbili na dunia kwa ujumla. Taarifa hiyo inasisitiza kuwa, China inashikilia mkakati wa kufanya mageuzi na kufungua mlango pamoja na kuongeza mahitaji kwenye soko la China.

    Taarifa hiyo imeainisha kuwa, makubaliano yangefikiwa kati ya China na Marekani kwa sharti la pande hizo kutafuta ufumbuzi na kutofanya vita vya kibiashara, na ikiwa Marekani itatoa hatua za vikwazo vya kibiashara ikiwemo kuongeza kutoza ushuru wa forodha, makubaliano yaliyofikiwa hatayafanya kazi wala kutekelezwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako