• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomi wasema madajiliano endelevu ni ufunguo kwa China na Afrika kuingia zama mpya ya Ushirikiano

    (GMT+08:00) 2018-06-03 17:25:40

    Washiriki wa baraza la 20 la Wanshou mjini Nairobi nchini Kenya, wamesema kuna haja ya China na Afrika kufanya majadiliano endelevu ambayo yataimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili na kutoa mwelekeo wa pamoja katika siasa za kimataifa.

    Zaidi ya wasomi 50, kutoka China na Kenya walishiriki baraza hilo ambalo liliangazia zaidi kutafuta njia bora za kujenga jamii yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu kati ya China na Afrika kupitia ushirikiano wa pande nyingi ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya pendekezo la ukanda mmoja na njia moja.

    Ofisa Mwandamizi wa Ubalozi wa China nchini Kenya, Bw. Li Xuhang amesema uimara wa mashauriano na mabadilishano ya uelewa wa mambo utaufanya ushirikiano wa China na Afrika uingie kwenye zama mpya wa kunufaishana.

    Bw. Li amesema, China na Afrika zimeingia katika zama mpya yenye fursa mpya na mahitaji mapya, hivyo China inaihitaji Afrika kuliko ilivyokuwa hapo awali, na Afrika inaihitaji China kuliko zamani pia.

    Aidha Bw. Li aliongeza kuwa China na Afrika zinapaswa kuendeleza mbele ushirikiano imara katika kushughulikia malengo yanayofanana, mfano ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na uhifadhi wa mazingira.

    Kwa upande wao washiriki wa baraza hilo walisifu waratibu na utaratibu wa majadiliano hayo ambayo wamesema yatakuza ushirikiano kati ya China na Afrika, ikiwa ni muda mfupi kuelekea mkutano mkuu wa FOCAC mjini Beijing mwezi Septemba mwaka huu.

    Pia wakisema pendekezo la Ukanda mmoja na njia moja litaisaidia Afrika kwa kuijengea uwezo wa kujiendeleza, kuipa Afrika mafunzo ya utaalamu na mabadilishano ya ufahamu na ubunifu utakaosaidia maendeleo ya uchumi barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako