• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yaweka pingamizi dhidi ya maoni ya mjumbe wa Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-06-03 18:50:29

    Serikali ya Burundi imeratibu mpango wa nchi nzima wa kumpinga mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bw. Michael Kafando, kutokana na kauli yake ya hivi karibuni kuwa mabadiliko ya katiba nchini Burundi yatafanya hali ya kuwa mbaya zaidi.

    Utekelezaji wa Pingamizi hilo la wazi, ambao umefanyika katika miji mikuu yote ya majimbo 18 ya Burundi, sambamba na Bw. Kafando, ulifanyika pia dhidi ya serikali za Ufaransa na Ubeligiji kwa madai ya kuwagawa wananchi wa Burundi kufuatia maoni yao juu ya matokeo ya kura za maoni kwa ajili ya mabadiliko ya katiba.

    Alhamisi iliyopita mahakama ya katiba ya Burundi ilitangaza matokeo ya kura za maoni zilizofanyika mei 17 kuhusu kuongeza muhula wa Rais wa kukaa madarakani, kutoka miaka mitano hadi miaka 7, na unaomruhusu Rais kuhudumu kwa vipindi viwili mfululizo.

    Mahakama hiyo ilitangaza kuwa kura za ndiyo zilikuwa asilimia 73.24 na kura za hapana zilikuwa chache kiasi ya asilimia 19.37.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako