• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuondoa tangazo la hali ya hatari kufuatia kurejea utulivu wa kisiasa, na usalama

    (GMT+08:00) 2018-06-03 18:56:35

    Serikali ya Ethiopia jana imepitisha muswada wa kuondoa hali ya hatari ya miezi iliyotangazwa katikati ya mwezi Februari mwaka huu.

    Katika kikao chake kilichofanyika jana, Baraza la Mawaziri liliamua kuondoa tangazo hilo kabla ya muda wake kufika, kwa kile kinachodaiwa kuwa hali ya utulivu imerejea kwenye siasa na usalama nchini humo.

    Hali hiyo ya dharura kwa miezi sita ya kisheria, ambayo pia ilikuwa na uwezekano wa kuongezwa muda endapo hali ya usalama isingeimarishwa, ilitangazwa na baraza la mawaziri Februari 16, na baadaye ikapitishwa na Bunge baada ya siku 15.

    Baada ya Baraza la mawaziri kupendekeza Muswada wa kuondoa tangazo la hali hiyo ya hatari, muswada huo sasa unatarajiwa kupelekwa bungeni kwa ajili ya kupitishwa.

    Tangazo la hali ya hatari nchini Ethiopia lilitolewa baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hailemariam Desalegn kujiuzulu wadhifa wake, ambapo mambo kadhaa yalizuiliwa ikiwemo kumiliki silaha katika maeneo ya wazi au kugawa silaha kwa watu wengine, vile vile kusaidia shughuli ambazo zinahatarisha amani na usalama wa raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako