• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwendo wa mageuzi ya China hautabadilika

    (GMT+08:00) 2018-06-03 19:02:27

    Gazeti la Economic Daily na gazeti la Global Times la China leo, yametoa makala zinazoeleza kuwa, mageuzi na kufungua mlango na kupanua mahitaji ya ndani ni mkakati wa taifa wa China, mwendo huo wa China hautabadilika, pande mbili za China na Marekani zinapaswa kufanya juhudi kufikia mafanikio, lakini pia Marekani haingekuwa na wazo lisiloendana na hali halisi.

    Gazeti la Economic Daily linasema kuwa, zipo sababu tatu za kutobadilika kwa mwendo wa mageuzi na kufungua mlango wa China.

    Kwanza mwendo wa kuzidisha mageuzi na kufungua mlango ni chaguo la lazima linaloendana na mahitaji halisi ya maendeleo ya China. Hivi sasa bidhaa kutoka nje ni nyongeza muhimu ya utoaji bidhaa kwenye soko, wateja wa China wana uhitaji mkubwa wa bidhaa kutoka nje.

    Pili, mwendo wa kuzidisha mageuzi na kufungua mlango pia unaonyesha wazo la maendeleo ya kunufaishana la China. Kuongeza uagizaji bidhaa kutoka nje kunaonyesha nia ya dhati ya serikali ya China kufungua soko lake kwa dunia, na kuonyesha majukumu yake ikiwa nchi kubwa ya kuhimiza utandawazi wa uchumi wa kimataifa.

    Tatu, kuzingatia mwendo wa mageuzi na kufungua mlango wa China chini ya mazungumzo ya uchumi na biashara kati ya China na Marekani, kunaona vizuri zaidi nia na imani ya China ya kufungua mlango kwa kiwango cha juu zaidi.

    Kwa upande wake Gazeti la Global Times lenyewe limeandika kuwa, baada ya China na Marekani kufanya mazungumzo ya uchumi na biashara, zimepata maendeleo na kuanzisha nafasi kubwa ya ushirikiano wa kunufaishana. Kama makubaliano yaliyofikiwa mjini Washington yatatekelezwa, yatasaidia nchi hizo mbili na wananchi wake kutimiza hali ya kunufaishana kihalisi.

    Pia linasema kuwa, hali yenye utata ya mazungumzo hayo imeonyesha kuwa, bado kuna hali isiyo tulivu ya uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili kutokana na Marekani kuvunja ahadi yake. Kama Marekani itaanzisha tena hatua yoyote ya vita vya biashara, makubaliano yaliyofikiwa na pande hizo mbili yatafutwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako